NA GODFREY NNKO
LEO Dola ya Australia (AUD) inanunuliwa kwa shilingi 1700.34 na kuuzwa kwa shilingi 1718.5 huku Pula ya Botswana (BWP) inanunuliwa kwa shilingi 197.6 na kuuzwa kwa shilingi 200.3.
Yen ya Japan (JPY) inanunuliwa kwa shilingi 18.22 na kuuzwa kwa shilingi 18.4 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 155.96 na kuuzwa kwa shilingi 157.45.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Aprili 19, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65 huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.
Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2287.25 na kuuzwa kwa shilingi 2310.12 huku Paundi ya Uingereza (GBP) ikinunuliwa kwa shilingi 2996.52 na kuuzwa kwa shilingi 3027.41.
Aidha,Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2483.5 na kuuzwa kwa shilingi 2509.25 huku Yuan ya China (CNY) ikinunuliwa kwa shilingi 358.8 na kuuzwa kwa shilingi 362.3.
Kwa mujibu wa BoT, shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.8 na kuuzwa kwa shilingi 19.9 huku Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.23 na kuuzwa kwa shilingi 2.29.
Dirham (AED) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inanunuliwa kwa shilingi 622.8 na kuuzwa kwa shilingi 628.9 huku sarafu ya Austria ya Schilling (ATS) inanunuliwa kwa shilingi 146.8 na kuuzwa kwa shilingi 148.1.
Kwa mujibu wa Benki Kuu, dola ya Canada (CAD) inanunuliwa kwa shilingi 1818.6 na kuuzwa kwa shilingi 1836.2 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.06 na kuuzwa kwa shilingi 50.51.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania