NA GODFREY NNKO
LEO Yen ya Japan (JPY) inanunuliwa kwa shilingi 17.50 na kuuzwa kwa shilingi 17.67 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 143.84 na kuuzwa kwa shilingi 145.14.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Aprili 29, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65 huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.
Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2287.4 na kuuzwa kwa shilingi 2310.3 huku Paundi ya Uingereza (GBP) ikinunuliwa kwa shilingi 2851.3 na kuuzwa kwa shilingi 2880.7.
Aidha,Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2402.24 na kuuzwa kwa shilingi 2427.2 huku Yuan ya China (CNY) ikinunuliwa kwa shilingi 345.9 na kuuzwa kwa shilingi 349.2.
Kwa mujibu wa BoT, shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.8 na kuuzwa kwa shilingi 19.9 huku Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.23 na kuuzwa kwa shilingi 2.29.
Dirham (AED) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inanunuliwa kwa shilingi 622.8 na kuuzwa kwa shilingi 628.9 huku sarafu ya Austria ya Schilling (ATS) inanunuliwa kwa shilingi 146.8 na kuuzwa kwa shilingi 148.1.
Kwa upande wa Dola ya Australia (AUD) inanunuliwa kwa shilingi 1623.6 na kuuzwa kwa shilingi 1640.1 huku dola ya Canada (CAD) inanunuliwa kwa shilingi 1778.4 na kuuzwa kwa shilingi 1795.6 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.06 na kuuzwa kwa shilingi 50.51.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania