*Dola ya Australia (AUD) inanunuliwa kwa shilingi 1743.98 na kuuzwa kwa shilingi 1762.6
NA GODFREY NNKO
LEO shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65 huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.
Yen ya Japan (JPY) inanunuliwa kwa shilingi 18.6 na kuuzwa kwa shilingi 18.8 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 157.16 na kuuzwa kwa shilingi 158.6.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Aprili 6, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2287.2 na kuuzwa kwa shilingi 2310.1 huku Paundi ya Uingereza (GBP) ikinunuliwa kwa shilingi 3002.4 na kuuzwa kwa shilingi 3033.11.
Aidha,Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2506.53 na kuuzwa kwa shilingi 2532.52 huku Yuan ya China (CNY) ikinunuliwa kwa shilingi 359.5 na kuuzwa kwa shilingi 363.006.
Kwa mujibu wa BoT, shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.9 na kuuzwa kwa shilingi 20.04 huku Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.21 na kuuzwa kwa shilingi 2.28.
Dirham (AED) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inanunuliwa kwa shilingi 622.8 na kuuzwa kwa shilingi 628.8 huku sarafu ya Austria ya Schilling (ATS) inanunuliwa kwa shilingi 146.8 na kuuzwa kwa shilingi 148.1.
Kwa upande wa Dola ya Australia (AUD) inanunuliwa kwa shilingi 1743.98 na kuuzwa kwa shilingi 1762.6 huku Pula ya Botswana (BWP) inanunuliwa kwa shilingi 198.98 na kuuzwa kwa shilingi 201.9.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania