NA DIRAMAKINI
CHAMA cha Wamachinga Mkoa wa Dar es Salaam, wamekanusha taarifa iliyosambaa mtandaoni iliyotolewa na Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania kuhusu kutoshiriki kwa wamachinga kwenye Maonesho ya Biashara yanayotarajia kufanyika hivi karibuni kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa, taarifa hiyo imeleta taharuki kwa wananchi walio wengi hivyo taarifa kama hiyo ingetakiwa itolewe na Mamlaka ya Biashara TAN TRADE.
"Niseme kuwa sisi kama wamachinga wa Mkoa wa Dar es Salaam tulishiriki mwaka jana katika maonyesho tulikipia kiingilio cha laki moja na tukapewa meza kiti na kitambulisho hivyo taarifa hizo zilizosambaa siyo za ukweli zipuuzwe kiingilio hakijapanda kufikia kiasi hicho,"amesema Namoto.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Wamachanga Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Masoudy Chauka ametoa taarifa kwa viongozi wote wa wamachinga kuwepo kwa mfumo data wa machinga pamoja na mfumo wa Saccos ili kuwatambua wamachinga wote na kutatua changamoto zinazowakabili.