*Bilioni 271/- kufanikisha utekelezaji wake katika mikoa tisa
NA OR-TAMISEMI
SERIKALI ya Tanzania kwa ikishirikiana na Serikali ya Uingereza imezindua mpango wa elimu bunifu wa shule bora wenye thamani ya Shilingi bilioni 271 utakaosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia, ujumuishi na usalama kwa wasichana na wavulana katika shule za msingi nchini.


Akizungumza baada ya kuzindua mpango huo, Vicky amefurahia kwa kufanikishwa kwa mchakato huo, akisema ni mwanzo mzuri mpya wa ushirikiano katika sekta ya elimu kati ya Serikali ya Uingereza na Tanzania. Amesema, mradi huo utawanufaisha wanafunzi milioni 4 katika mikoa tisa.
Kwa upande wake, Silinde amesema," jukumu langu ni kuishukuru Serikali ya Uingereza na tunakushuru Waziri (Vicky) kwa ujio wako Tanzania na hatua ya Serikali yako kutusaidia kwenye sekta ya elimu.
"Ahadi yetu ni fedha zote zitakazoletwa zitatumika malengo yaliyokusudiwa," amesema Silinde.
Naye, Profesa Mkenda amesema, mradi huo utatekelezwa katika mikoa tisa na utaboresha mazingira ya ufundishaji wa darasani pamoja kuwaendeleza walimu ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.