Watumishi Wizara ya Madini watoa tabasamu kwa yatima kuelekea Sikukuu

NA TITO MSELLEM-WM

KATIKA kuelekea Sikukuu ya Pasaka, watumishi wa Wizara ya Madini wameungana pamoja kuwatembelea na kutoa msaada watoto yatima wa Kituo cha Tumaini Jema na Kituo cha Watoto cha Nyumba ya Matumaini vilivyopo jijini Dodoma.
Vituo hivyo, vyenye watoto yatima vina mahitaji makubwa ambapo Kituo cha Tumaini Letu kina watoto 18 na Kituo cha Watogto cha Nyumba ya Matumaini kina watoto 62 ambao wazazi wao walipoteza maisha kutakana na janga la virus vya UKIMWI.
Akizungunza kwa niaba ya watumishi wa Wizara ya Madini, Kamishna Msaidizi Undelezaji Migodi, Theresia Ntuke amesema watumishi wa wizara hiyo wameguswa na kuamua kutoa msaada kwa watoto yatima ikiwa ni sehemu ya kutenda matendo ya huruma.

“Kwa niaba ya Watumishi wenzangu wa Wizara ya Madini, naomba niwapongeze watoa huduma wote wa kituo hiki kwa kazi kubwa mnayoifanya, naomba muendelee na moyo huo na Mwenyezi Mungu azidi kuwabarki,” amesema Ntuke.

Kwa upande wake, Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Watoto cha Nyumba ya Matumaini, Sista Aurea Kiara amesema, kituo anachokisimamia kinapokea watoto kuanzia miaka mitatu ambao wazazi wao wamefariki kwa ugonjwa wa Ukimwi pamoja na watoto wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ambao wametengwa na familia zao.
Aidha, Sista Kiara amewashukuru watumishi wa Wizara ya Madini na kuwatakia Maadhimisho mema ya Sikukuu ya Pasaka ambapo amewataka kuendelea na moyo huo na Mwenyezi Mungu atawazidishia pale wanapotoa.

Naye, Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Tumaini Jema Exusuper Liyumba amesema kituo anacho liongoza kina jumla ya watoto 18 ambapo hadi sasa kituo kimepata eneo Msalato ambapo kitajengwa kituo kikubwa chenye uwezo wa kuhudumia watoto zaidi ya 128.
Katika kuungana na jamii Wizara ya Madini imekuwa ikishirikiana na vituo mbalimbali vya kuhudumia jamii kwa lengo la kushikana mkono na kupeana faraja katika maisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news