NA DIRAMAKINI
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amekutana na kuongea na Wanajeshi wastaafu kutoka jimbo la Uchaguzi la Kawe jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuangalia namna ya kuzitatua.
Akiongea na wastaafu hao Mheshimiwa Waziri alianza kwa kumshukuru Mheshimiwa Askofu Gwajima kwa kufanikisha mkutano wake na Wastaafu kutoka jimboni kwake. Aidha, alimshukuru Mheshimiwa Rais kwa jitihada zake za kuhakikisha watu wake wako vizuri.
Mheshimiwa Dkt. Stergomena alibainisha wazi kuwa umuhimu wa mkutano na wastaafu hao kwani umemuwezesha kukutana, kubadilishana nao mawazo na pia kuangalia mfumo mzuri utakaowawesha wastaafu hao kutoa hoja zao kwa lengo la kutatua changamoto zao.
Aidha, Waziri wa Ulinzi na JKT aliwahakikishia wastaafu hao kuwa Wizara yake na serikali kwa ujumla inawathamini wastaafu na inazifahamu Changamoto zote zinazowakabili na tayari baadhi ya changamoto mchakato wa kuzifanyia kazi umeshaanza na kuwaahidi kuwa Wizara inazichukua changamoto zilizowasilishwa katika mkutano huo amezichukua.
Kwa upande wake, Mheshimiwa Askofu Gwajima akiongea kwenye Mkutano huo, amemshukuru Mhshimiwa Rais kwa maelekezo yake yanayowataka viongozi katika maeneo yao kuwasiliza wastaafu wote katika maeneo yao. “Namshukuru Mheshimiwa rais kwa maelekezo yake ya kututaka tuwasikiliza, kuwajali na kuwasaidia wastaafu wote katika maeneo ya Majimbo yetu,”amesema.