NA HAPPINESS SHAYO-WMU
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka wananchi wanaoilalamikia Serikali kuhusu kurejeshewa mifugo iliyokamatwa hifadhini kuwasilisha maombi yao Wizara ya Maliasili na Utalii ili yafanyiwe kazi.
Ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali na Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina.
“Endapo kuna wananchi ambao mifugo yao ilikamatwa na mahakama kuamuru kurejeshwa mifugo yao na hawajarejeshewa wawasilishe malalamiko yao Wizara ya Maliasili na Utalii ili yashughulikiwe,” Mhe. Masanja amesisitiza.
Aidha, amewataka wananchi hususan wafugaji kuacha kuingiza mifugo kwenye maeneo ya Hifadhi kwani kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 ni kosa kuingiza na kuchunga mifugo ndani ya hifadhi.