Yanga SC ileee!!!, yaipindua Azam FC kijeshi

NA DIRAMAKINI

BAO la dakika 11 lililotupiwa nyavuni na Dodgers Kola wa Azam FC dhidi ya Yanga SC halikuwa si kitu kwa Wanajangwani, kwani baada ya kuitazama ramani waliamua kupindua matokeo hayo.

Ni kupitia mtanange wa nguvu ambao ni mwendelezo wa michuano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopiigwa katika dimba la Azam Complex lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Djuma Shabani ndani ya dakika 17 aliwanyanyua Wanajangwani kwa kusawazisha bao kupitia mkwaju wa penalti kabla ya Fiston Mayele kurejea katika nyavu za Azam dakika ya 76 ya mchezo huo.

Matokeo hayo yanawafanya Yanga SC kuendelea kushikilia rekodi ya kutokufungwa msimu huu ikifikisha alama 51, baada ya kucheza michezo 19.
Ni baada ya kushinda ikianza na Mtibwa Sugar kwa kipigo cha 2-0, Kagera Sugar kwa kipigo cha 3-0, Geita Gold kwa kipigo cha 1-0, KMC kwa kipigo cha 2-0 na 2-1 kutoka kwa Azam FC leo.

Huku Azam FC inaendelea kushikilia nafasi ya tatu kwa alama 28, baada ya kucheza michezo 19, huku kikiwa ni kipigo cha pili kutoka kwa Yanga kufuatia mzunguko wa kwanza kufungwa mabao 2-0, Oktoba 30,mwaka jana.

Aidha, bao hilo kwa Mayele linamfanya kuwa kileleni mwa ufungaji bora, kwani hadi sasa anafikisha mabao 11, akiwaacha Reliants Lusajo wa Namungo FC mwenye mabao 10 na George Mpole wa Geita Gold FC mwenye mabao tisa hadi sasa.

Azam FC katika mtanage huo, dakika ya 55 ilifanya mabadiliko ya kumtoa Charles Zulu aliyepata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Tepsie Evance huku dakika ya 60, Yanga ilimtoa Dickson Ambundo aliyeonekana kuchoka huku nafasi yake ikichukuliwa na Crispin Ngushi ambaye kwa muda mrefu alikuwa akiuguza majeraha.

Pia Yanga ilimtoa Denis Nkane na nafasi yake kuchukuliwa na Heritier Makambo ili kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji wakati Azam FC iliwaingiza Pascal Msindo, Ayoub Lyanga na Idris Mbombo kuimarisha safu ya ushambuliaji na ulinzi.

Mbali na mchezo huo, katika dimba la Nyamagana jijini Mwanza, Biashara United imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news