NA DIRAMAKINI
KATIKA kuhakikisha uwazi na haki kwenye uendeshaji wa shughuli za uchaguzi katika matawi ya Yanga na kwa kuzingatia matakwa ya Ibara ya 45 (2) ya Katiba ya Yanga, Kamati ya Uchaguzi imeridhia kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika uchaguzi mpaka pale klabu itakapoandaa kanuni zake.