NA DIRAMAKINI
TUNAKUKARIBISHA, bila shaka na mwelekeo wa safari hii nchini Marekani, ni pamoja na kuzingatia fursa za uwekezaji kama inavyohusiana na uchumi kama suala la jumla, lakini pia katika eneo la utalii.
Na safari yako pia imezalisha karibu dola bilioni moja katika uwekezaji mpya kutoka kwa makampuni nchini Marekani. Na hilo litachangia, bila shaka katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania, lakini kwa njia hiyo, litachangia ukuaji ukuaji wa uchumi na ajira nchini Marekani pia.Soma kwa kina hapa>>>
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wafanyabiashara, Wawekezaji pamoja na Wadau Wakuu wa Sekta ya Habari wa nchini Marekani katika Jiji la New York leo tarehe 18 Aprili, 2022. (Picha na Ikulu).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Meya wa Jiji la New York Mhe. Eric Adams mara baada ya mazungumzo yao leo tarehe 18 Aprili, 2022 nchini Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Meya wa Jiji la New York Mhe. Eric Adams kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Jiji hilo tarehe 18 Aprili, 2022 nchini Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Meya wa Jiji la New York Mhe. Eric Adams Jijini humo nchini Marekani leo tarehe 18 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mwandaaji wa filamu ya Royal Tour na Baadhi ya Wafanya Biashara wa Nchini Marekani baada ya Futari Jijini New York Marekani.