NA DIRAMAKINI
HALMASHAURI ya Manispaa ya Tabora mkoani Tabora imeungana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mhe. Innocent Bashungwa kumpongeza Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Tabora Bi. Tumaini Mgaya kwa uongozi wake mahiri wa kuisimamia Idara ya Maendeleo ya Jamii.

Bi. Mgaya amekabidhiwa tuzo hiyo pamoja na shilingi milioni tatu. Awali, Waziri Bashungwa alieleza kuwa, kufanya hivyo kutatoa motisha kwa wengine kufanya kazi kwa bidii, umoja na mshikamano lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.