NA DIRAMAKINI
WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam wamesema kuwa,ni jukumu la kila mwendesha chombo cha moto barabarani kuhakikisha anazingatia kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kuepusha ajali za mara kwa mara ambazo licha ya kusababisha vifo, majeruhi, uharibifu wa vyombo vya moto pia ni moja wapo ya chanzo kikuu cha kuvutia umaskini.

Ajali hiyo ambayo imehusisha magari kadhaa kutokana na kutoelewana baina ya madereva huku kila mmoja akijiona yeye ndiye mwenye haki zaidi ya mwingine, ingawa haijasababisha vifo au majeruhi, lakini imesababisha uharibifu wa vyombo hivyo vya moto.

"Hii kiuchumi inaashiria nini? Inaashiria tukishindwa kuzuia au kuzingatia kanuni za usalama barabarani kamwe hatutaweza kupata maendeleo endelevu, nitumie muda huu kuwashauri wenzangu, tuheshimu sheria za usalama barabarani, kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeipa heshima familia, jamii na Taifa.
"Gharama zinazopaswa kutumika kwa ajili ya kugharamia majeruhi au kwa namna nyingine ile zitatumika kwa shughuli nyingine za maendeleo,"amesema Amos Justine mkazi wa Jiji la Dar es Salaam ambaye amezungumza na DIRAMAKINI muda mfupi baada ya kutokea ajali hiyo.
Kwa upande wake,Munira amesema kuwa,ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anazingatia usalama barabarani kwani, inapotokea ajali mara nyingi huwa yanajitokeza mambo ya ovyo.
"Kuna mambo ya ovyo ovyo ambayo ajali ikitokea huwa yanajitokeza mfano kutoleana lugha chafu, wengine kama hao unaowaona hapo si wote ni wema, wanaangalia namna ya kupata upenyo ili walau wapate chochote kitu humo ndani (udokozi), hivyo tukiwa barabarani tuhakikishe tunazingatia suala la usalama barabarani,"anasema Munira.
HIZI HAPA NAMBA ZA MAKAMANDA WA POLISI NA WAKUU WA USALAMA BARABARANI KWA MIKOA YA TANZANIA BARA;