NA MWANANCHI
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewafutia kesi ya Uhujumu Uchumi na kuwaachia huru wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini Tanzania (TMDA) akiwemo Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula, Raymond Wigenge, waliokuwa wanakabiliwa na shtaka moja la kuisababishia hasara mamlaka hiyo ya Shilingi milioni 58.
Hiyo ni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuieleza mahakama kuwa hana nia ya kuendelea na kesi dhidi ya washtakiwa hao.
Uamuzi wa kuifuta kesi hiyo umetolewa leo Mei 17, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Ritha Tarimo, wakati shauri hilo lilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.