NA DIRAMAKINI
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Monduli Mkoa wa Arusha, Bw. Raphael Siumbi amesema hafahamu kadhia inayowakabili wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nanja ambao wamelalamikia kitendo cha kupewa kazi ya kuchota maji wakati wa masomo.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wanahabari ambao walitaka kufahamu kadhia hiyo ya wanafunzi kuchota maji wakati wa masomo ambapo amesema, yeye muda mwingi yupo ofisini, hivyo kutambua tatizo hilo ni vigumu hadi apewe taarifa.
"Siwezi kufahamu sababu nipo ofisini linaweza tokea jambo Engaruka mimi nitalijuaje nipo huku au aliye Engaruka hajanijulisha mpaka...unless niwe Nabii nikilala usingizini nitaota kuna mahali kitu kinaendelea.
"Ni suala la mtu aliyeona aniambie sasa huyo aliyeona ni mtu wa aina gani na tabia zake, uzalendo au ufahamu wake siwezi kumhukumu ni nani na yukoje jambo la hakika sina taarifa....
"Ndio nimelisikia kama unavyoona tuko bize ndani huko tangu asubuhi kwa hiyo ndio nimelisikia maanake nitalifanyia kazi kuona manaake ndio umenipa taarifa tunasema ni nnatural justice nitasikiliza na upande wa pili au nitafanya uchunguzi nini kimetokea huko na kwa nini kwamba Watoto wanaweza wasiingie darasani kwanza wachote maji," amesema Raphael.