NA DIRAMAKINI
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini ( LATRA) imetangaza kuanza kutumika kwa nauli mpya za mabasi na daladala badala ya Mei 14,2022 kutokana kupanda kwa bei ya mafuta.
Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabara, Johansen Kahatano alikaririwa jana akisema kuwa,watoa huduma wanapaswa kubandika nauli hizo ndani ya mabasi na katika vituo vya kukatia tiketi na wale wa daladala wabandike ubavuni karibu na mlango na kutoa tiketi zenye nauli mpya.Soma hapa>>>
Hivi karibuni, LATRA ilitangaza bei mpya za nauli za mabasi na daladala nchini ambazo zilipaswa kutumika kuanzia Mei 14,2022 lakini kutokana na kupanda kwa mafuta bei hizo zimeanza kutumika,
Nauli za mabasi yaendayo mikoani zimepanda kwa daraja la kawaida ni sh. 41.29 kwa kilomita moja kutoka sh.36.89 huku daraja la kati likipanda kwa shilingi 56.88 kutoka sh.53.22 na nauli kwa wanafunzi imebakia kuwa sh. 200 kwa daladala.