NA INNOCENT KANSHA-Mahakama
JAJI Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe.Dkt. Adam Mambi amewaomba na kuwasisitiza Wahasibu na Wakaguzi wa ndani kuzingatia malengo ya mafunzo kwa vitendo watakaporudi vituoni kutekeleza majukumu yao.
Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Adam Mambi (katikati) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani (hawapo katika picha) leo tarehe 30, Mei 2022 katika Ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Jijini Dodoma. Amesisistiza uwazi, nidhamu na uwajibikaji katika kuwahudumia wananchi, wengine ni Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Bernard Mpepo (kulia) na kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, Bw. Sumera Manoti.
Akifungua rasmi mafunzo Wahasibu
na Wakaguzi wa ndani Mei 30, 2022 katika Ukumbi wa Kituo Jumuishi cha
Utoaji Haki Jijini Dodoma, Mhe. Dkt. Mambi amesema mafunzo hayo ni
muhimu kama sehemu ya utekelezaji wa sera, sheria zinazosimamia masuala
ya fedha na hususani katika kipindi hiki ambacho Mahakama ya Tanzania
inatekeleza Mpango Mkakati wa Awamu ya pili wa 2020/21 hadi 2024/2025.
“Wahasibu
na Wakaguzi wa ndani wote ninyi ndiyo wasimamizi wakuu wa kusimamia
namna bora ya matumizi ya fedha ama nidhamu ya pesa za Umma, kwa lugha
nyingine nyie ni wasaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),”amesema Jaji Mambi. Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya Waasibu na wakaguzi wa ndani wa Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza Mwezeshaji (hayupo katika picha) leo tarehe 30, Mei 2022 katika Ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Jijini Dodoma.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Mchumi kutoka Idara ya Mipango na Ufuatiliaji ya Mahakama ya Tanzania, Bw. Kisingi Mhando akitoa mada ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania Awamu ya Pili kwa washiriki hao.
Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Adam Mambi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo, wengine ni Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Bernard Mpepo (wa pili kulia) na kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, Bw. Sumera Manoti (wa pili kushoto), Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe.Sylivia Lushasi (wa kwanza kushoto) na Afisa Utumishi wa Mahakama ya Tanzania kutoka kitengo cha Mafunzo Bw.Rajab Singana (wa kwanza kulia).
Mhe.
Mambi, amesema kuwa, anaamini kuwa, kila mshiriki anatambua sera,
miongozo na sheria zinazosimamia matumizi bora ya fedha za umma. Hivyo,
anaamini kwamba, kupitia mafunzo hayo Maafisa hayo watajengewa uwezo,
kukumbushwa majukumu yao na kubadilishana uzoefu wa utendaji wa kila
siku.
Kwa
upande wa usimamizi wa rasilimali fedha, Jaji Mambi aliwakumbusha
washiriki wa mafunzo hayo kuwa shughuli nyingi za Serikali hasa za
usimamizi wa fedha zinafanyika kwa njia ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) ambayo imerahisisha kuongezeka kwa nidhamu, uwazi,
uwajibikaji na utambuzi wa matumizi usiofichika. “Natambua mifumo hii
mnaitumia kila siku katika kazi zenu ni rai yangu kwenu mzidi
kujiimarisha katika kuitumia ili kutatua changamoto mnazokabiliana
nazo”, alisisitiza Jaji Mambi.
Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Adam Mambi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo wa kada ya Wahasibu, wengine ni Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Bernard Mpepo (wa pili kulia) na kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma Bw. Sumera Manoti (wa pili kushoto), Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe.Sylivia Lushasi (wa kwanza kushoto) na Afisa Utumishi wa Mahakama ya Tanzania kutoka kitengo cha Mafunzo Bw.Rajab Singana (wa kwanza kulia).
Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Adam Mambi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo wa kada ya Wakaguzi wa ndani, wengine ni Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Bernard Mpepo (wa pili kulia) na kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma Bw. Sumera Manoti (wa pili kushoto), Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe.Sylivia Lushasi (wa kwanza kushoto) na Afisa Utumishi wa Mahakama ya Tanzania kutoka kitengo cha Mafunzo Bw.Rajab Singani (wa kwanza kulia).(Picha na Innocent Kansha -Mahakama).
Akifafanua
kuhusu Sheria ya mtandao inayotumiwa na Wahasibu, Jaji Mambi amesema,
Sheria ya Miamala ya Kielektroniki namba 13 ya mwaka 2015 inaelekeza
masuala mbalimbali ikiwemo malipo ya fedha kielekroniki, usimamizi wa
fedha na pia utekelezaji wa sheria ya miamala ya kielektroniki. Sheria
tajwa kifungu cha 13 na 15 ni vifungu vya muhimu sana katika utekelezaji
wa majukumu ya kiuhasibu hasa wanapofanya malipo kimtandao.
Kifungu
cha 13 cha sheria ya miamala ya kielektroniki namba 13 ya mwaka 2015
kinazungumzia zaidi serikali mtandao, kinatambua matumizi ya serikali
mtandao ama huduma za serikali mtandaoni (E-Government). Kifungu cha 15
cha sheria hiyo kinaelezea malipo na uwasilishaji wa stakabadhi
kielektroniki na hayo mambo ni ya msingi katika utekelezaji wa shughuli
za kihasibu, aliongeza Dkt. Mambi
Washiriki
wa mafunzo hayo ya Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wameombwa kutosita
kusambaza elimu waliyoipata kwa watumishi wengine ambao hawakupata
nafasi hiyo adhimu ya kushiriki ili kuwajengea uwezo na uelewa wa pamoja
katika kusukuma gurudumu la shughuli za taasisi.