NA DIRAMAKINI
NDIYO, kwa mujibu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) kuna aina mbalimbali za matibabu kwa waraibu wa dawa za kulevya ingawa hakuna tiba moja ambayo inafaa kwa waraibu wote.
DCEA inaeleza kuwa, matibabu ya uraibu wa dawa za kulevya hutofautiana sana kulingana na aina ya dawa husika, kiasi cha dawa kilichotumika, muda wa uraibu, matatizo ya kiafya na mahitaji ya kijamii na mtu binafsi.
Huduma za tiba ya uraibu zinazotolewa nchini ni;
>Tiba saidizi kwa waraibu kwa kutumia dawa (Medically Assisted Therapy - MAT)
>Huduma katika Nyumba za Upataji Nafuu (Sober Houses)
>Tiba kwenye vituo vya kutolea Huduma za Afya ya Akili.
Hata hivyo, kwa mujibu wa DCEA kuna baadhi ya waraibu wanaopatiwa huduma za unasihi pekee kwenye asasi za kiraia na kuachana na matumizi ya dawa hizo.