NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. John Jingu ameeleza kuwa uwepo wa Safari Chaneli ni fursa ya kipekee kuendelea kuitangaza nchi yetu ndani na nje na kuchagiza ukuaji wa uchumi.
“Safari chaneli ni moja ya nyenzo ya kukuza utalii wetu na sisi kama wadau tuna jukumu la kuhakikisha tunawekeza vya kutosha katika maeneo muhimu ikiwemo rasilimali fedha zitakazosaidia kuendesha chaneli hii ili malengo ya uwepo wake yatimie,”alisisitiza Dkt. Jingu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi alieleza kuwa uwepo wa chaneli hiyo utasaidia katika kuvutia na kuongeza hamasa kwa watalii kuingia nchini.
“Tanzania Safari Channel ni msaada katika kuutangaza utalii, na kuitangaza nchi yetu na hii ni fursa kwetu nitoe wito kwa taasisi mbalimbali kuendelea kutangaza na kuitumia fursa hii ili kuendelea kukuza uchumi wetu,”alieleza Dkt. Yonazi
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab alipongeza hatua ya uwepo wa chaneli ya hii, huku akieleza jitihada za Zanzibar kuanzisha chaneli ya utalii itakayosaidia kuitangaza na kuonesha vivutio vilivyopo.
“Kwa upande wa Zanzibar tuna mpango wa kuwa na chaneli ya ZBC 3 inayolenga kuonesha masuala ya utalii hatua hii inadhihirisha namna viongozi wetu kwa pande zote mbili wanavyojitahidi kutangaza vivutio vyetu vya utalii tunaahidi kuendelea kuwaunga mkono kwa kuhakikisha tunakuwa wabunifu katika kutangaza utalii wetu,”alisema Fatma.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara wadau wa Tanzania Safari Channel (TSC) wakifuatilia kikao hicho.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
Alihitimisha kuwa chaneli hizi zitasaidia kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu tamaduni zetu hivyo kudumisha.