Maajabu ya Mbunge aliyeruka sharakasi bungeni

NA MWANANCHI

MBUNGE wa Mbulu Vijijini (CCM) Flatei Massay ameruka sarakasi bungeni ikiwa ni kuonyesha msisitizo wa hoja yake kuwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imekuwa ikitoa ahadi ya ujenzi wa barabara ya Mbulu hadi Haydom bila utekelezaji.
Flatei ameruka sarakasi leo Jumatatu Mei 23, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka 2022/2023.

Flatei amesema licha ya kuahidiwa ujenzi wa barabara hiyo tangu katika bajeti ya mwaka jana, Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeonyesha fedha zilizotengwa mwaka jana zimepelekwa kulipa madeni.

Amesema katika kitabu cha bajeti cha mwaka huu imeonyeshwa kuwa barabara hiyo itajengwa katika kiwango cha lami lakini kwa Kilometa 25.

“Kama waliniahidi kuwa barabara itajengwa hilo tangazo linachukua muda gani? Mimi hapa mheshimiwa Spika sio shilingi tu. Mimi wananchi wameniambia shilingi niichukue nende nayo Mbulu Vijijini maana hapa hamna namna tena,” amesema.

Alimhoji Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kama hamtoi nje ya ukumbi wa Bunge basi apige sarakasi.

“Mimi naona wanataka kunitengenezea ajali kuliko kukitengenezea ajali chama changu si bora uruhusu tu niruke hapa ili wastuke sasa nitafanyaje sasa,”amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news