NA DIRAMAKINI
CHAMA cha Wasafirishaji Tanzania (TAT) wiki hii kiliandaa mkutano wa vyama vyote vya wasafirishaji kulaani vitisho vya baadhi ya madereva wao wanaotangaza kugoma kazi na kuiomba Serikali ichukue hatua za haraka, kwani kauli za madereva hao zinachochea vurugu na kudhoofisha jitihada za ujenzi wa uchumi.
Katika siku za karibuni baadhi ya madereva wakiwa safarini ndani na nje ya Tanzania, wamekuwa wakirusha mitandaoni sauti zao wakisema wanagoma kazi wakidai, pamoja na mambo mengine, kulipwa mishahara, posho za safari na kuongezewa mafuta, mambo ambayo Rais wa TAT, Mohammed Abdullah, amesema mengine ni ya kimkataba.
Aidha,yanazungumzika na hayahalalishi vitisho vya kutelekeza magari na mizigo, mali ambazo wamekabidhiwa na wameaminiwa wazitunze. Kwa kina tazama sehemu ya kwanza hadi ya mwisho ya video ya taarifa hii ambayo imeandaliwa kwa msaada wa TAT TV (ambayo karibuni itakuwa hewani);
TAZAMA VIDEO:SEHEMU YA 1-4 TAT