Mambo usiyoyafahamu kumuhusu Prof.Edward Hoseah aliyejitoa kuitumikia TLS

NA DIRAMAKINI

PROFESA Edward Hoseah ni miongoni mwa Watanzania wasikivu, wapole, wanyenyekevu na msomi anayependa kushikamana na wengine kwa ustawi bora wa kijamii na Taifa.
Akiwa ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ambaye anatetea kiti chake, Profesa Edward Hoseah amebobea katika sheria huku akijitolea kwa moyo wote kuitumikia taasisi hiyo.

Chama cha Sheria ya Tanganyika (TLS) ndicho chombo pekee cha kisheria kinachotoa msaada wa sheria na ni chama cha kitaaluma kinachowakilisha wanasheria (mawakili) nchini Tanzania.

SAFARI YA KITAALUMA

- Mwaka 1985, Profesa Hoseah alitunukiwa Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam, akishinda pia Tuzo ya Mwanafunzi Bora ya Kitivo cha Sheria katika "Constitution Law".

- Mwaka 1989 alitunukiwa Shahada ya Uzamili katika Sheria (LLM) ya Chuo Kikuu cha Queens, Ontario, nchini Canada na kutupewa Tuzo ya Mwanafunzi bora ya Chuo Kikuu cha Queens.

- Mwaka 2007 alitunukiwa Shahada ya Uzamifu (PhD) katika Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam akibobea katika "Law of Evidence".

- Mafunzo katika Sera, Uongozi, Maadili na Kukabiliana na Rushwa katika Vyuo na taasisi zifuatazo; *Chuo kikuu cha Passau (2007), Chuo kikuu cha Birmingham (2003) na Taasisi ya Benki ya Dunia (WI) mwaka 1998.

- Mwaka 1997 alihitimu Astashahada ya Utatuzi wa Migogoro kutoka katika Kituo cha Diplomasia (CFR) nchini Tanzania.

UZOEFU NA UBOBEZI KATIKA SHERIA

- Mhadhiri katika Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ( Law of Evidence and Legal Practice)

- Mhadhiri katika Kituo cha Diplomasia (CFR) akifundisha Sheria katika Biashara za Kimataifa na Uwekezaji.

- Mwanazuoni (Visiting Scholar) katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Northwestern, Chicago (2003-2005)

- Profesa wa muda (Adjunct Professor) wa Shule ya Sheria ya Duke nchini Marekani (2010-2012).

- Tuzo kutoka katika Taasisi ya kimataifa kwa mchango katika maboresho ya Sheria ya Jinai (2003).

- Wakili na Mkurugenzi katika Hosea & Co Advocates wabobezi na watoa huduma mbalimbali za kisheria.

- Mkufunzi wa Taasisi ya "Uongozi Institute" kuanzia mwaka 2019

- Profesa katika Chuo Kikuu cha Iringa kuanzia mwaka 2021

- Mwandishi wa vitabu na machapisho ya kitaaluma.

- Mjumbe wa Bodi mbalimbali na mshauri wa masuala ya kitaalam katika mawanda ya sheria. 

UZOEFU KATIKA SHUGHULI ZA UONGOZI

- Rais wa sasa wa Tanganyika Law Society (TLS) kuanzia mwaka 2021.

- Mkurugenzi wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania.

- Rais wa Mamlaka ya Kukabiliana na Rushwa Afrika Mashariki (2008-2010, 2014-2015).

- Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kukabiliana na Rushwa katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC ( SAFAC) mwaka 2010-2011.

- Mwenyekiti wa Bodi ya Umoja wa Afrika (AU) katika Mapambano ya Rushwa (2011-2012)

 - Makamu wa Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Kukabiliana na Rushwa (IAACA, 2012-2015).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news