NA DIRAMAKINI
PROFESA Edward Gamaya Hoseah ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ambaye anamaliza muda wake huku akiomba ridhaa tena ya kutetea nafasi hiyo kupitia uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika ndani ya mwezi huu.
Akiwa amewahi kuhudumu katika utumishi wa umma kwa miaka zaidi ya 35 kabla ya kustaafu mwaka 2015 na kuendelea na majukumu mengine ya kisheria akiwajibika kama Mshirika Msimamizi katika Hoseah & Co Advocates jijini Dar es Salaam, uchaguzi wa mwaka jana aliibuka kidedea kwa kura 297 na kuwashinda wenzake wanne aliokuwa akichuana nao.
Miongoni mwa aliokuwa akichuana nao ni wakili Albert Msando, Shehzad Wall, Rais wa zamani wa chama hicho, Francis Stolla na mwanamke pekee Flaviana Charles.
Akiwa amewahi kuhudumu katika utumishi wa umma kwa miaka zaidi ya 35 kabla ya kustaafu mwaka 2015 na kuendelea na majukumu mengine ya kisheria akiwajibika kama Mshirika Msimamizi katika Hoseah & Co Advocates jijini Dar es Salaam, uchaguzi wa mwaka jana aliibuka kidedea kwa kura 297 na kuwashinda wenzake wanne aliokuwa akichuana nao.
Miongoni mwa aliokuwa akichuana nao ni wakili Albert Msando, Shehzad Wall, Rais wa zamani wa chama hicho, Francis Stolla na mwanamke pekee Flaviana Charles.
SAFARI YA KITAALUMA
Profesa Hoseah mwaka 1985 alitunukiwa Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, akishinda pia Tuzo ya Mwanafunzi Bora ya Kitivo cha Sheria katika "Constitution Law".
- Mwaka 1989 alitunukiwa Shahada ya Uzamili katika Sheria (LLM) ya Chuo Kikuu cha Queens, Ontario, nchini Canada na kupewa Tuzo ya Mwanafunzi Bora ya Chuo Kikuu cha Queens.
- Mwaka 2007 alitunukiwa Shahada ya Uzamifu (PhD) katika Sheria ya Chuo kikuu cha Dar es salaam akibobea katika "Law of Evidence".
- Mafunzo katika Sera, Uongozi, Maadili na Kukabiliana na Rushwa katika Vyuo na Taasisi zifuatazo; Chuo Kikuu cha Passau (2007), Chuo kikuu cha Birmingham (2003) na Taasisi ya Benki ya Dunia (WI) mwaka 1998.
- Mwaka 1997 alihitimu Astashahada ya Utatuzi wa Migogoro kutoka katika Kituo cha Diplomasia (CFR) nchini Tanzania.
UZOEFU NA UBOBEZI KATIKA SHERIA
- Mhadhiri katika kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Cha Dar es salaam ( Law of Evidence and Legal Practice)
- Mhadhiri katika Kituo cha Diplomasia (CFR) akifundisha Sheria katika Biashara za kimataifa na uwekezaji.
- Mwanazuoni (Visiting Scholar) katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Northwestern, Chicago (2003-2005)
- Profesa wa muda (Adjunct Professor) wa Shule ya Sheria ya Duke Nchini Marekani (2010 - 2012).
- Tuzo kutoka katika Taasisi ya kimataifa kwa mchango katika maboresho ya Sheria ya Jinai (2003).
- Wakili na Mkurugenzi katika Hosea & Co Advocates wabobezi na watoa huduma mbalimbali za kisheria.
- Mkufunzi wa Taasisi ya "Uongozi Institute" kuanzia mwaka 2019
- Profesa katika Chuo Kikuu cha Iringa kuanzia mwaka 2021
- Mwandishi wa vitabu na machapisho ya kitaaluma.
- Mjumbe wa Bodi mbalimbali na mshauri wa masuala ya kitaalam katika mawanda ya Sheria.
UZOEFU KATIKA SHUGHULI ZA UONGOZI
- Rais wa sasa wa Tanganyika Law Society (TLS) kuanzia mwaka 2021.
- Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania.
- Rais wa Mamlaka ya Kukabiliana na Rushwa Afrika Mashariki (2008-2010, 2014-2015).
- Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kukabiliana na Rushwa katika Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC ( SAFAC) mwaka 2010-2011.
- Mwenyekiti wa Bodi ya Umoja wa Afrika (AU) katika Mapambano ya Rushwa (2011-2012)
- Makamu wa Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Kukabiliana na Rushwa (IAACA, 2012-2015).