MTIHANI MWEMA:Chuo chenu cha Huria, Hapa kwetu Tanzania, Mema kinawatakia

NA DKT.MOHAMED OMARY MAGUO

KESHO Mei 9, 2022 Watahiniwa 95,955 kutoka shule za sekondari 841 na vituo vya kujitegemea 250 wanatarajia kuanza mitihani yao ya kumaliza Kidato ya Sita ambao unatarajiwa kumaliza Mei 27,2022.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dkt.Charles Msonde wakati akizungumza na waandishi wa habari leo amefafanua kuwa, pia watahiniwa 9,670 kutoka vyuo 70 wamesajiliwa kufanya mitihani ya mwisho ya kozi ya ualimu katika ngazi ya Stashahada na cheti.
Amesema, kati ya watahiniwa wa Kidato cha Sita 85,531 ni wale wa shule na 10,424 ni wa kujitegemea.

Mshairi wa Kisasa ambaye pia ni Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dkt. Mohamed Omary Maguo kupitia ubobezi wake katika utunzi wa mashairi, ametunga utenzi maalum kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa ajili ya kuwatakia heri na baraka watahiniwa wote wa mitihani hiyo kama ifuatavyo;

1:Kwa baraka za Jalia
Mtihani mewadia
Form Six Tanzania
Heri nyingi watakia

2:Siha njema na afia
Maradhi kutofikia
Amani kutawalia
Siku zote 'paka mwisho

3:Ukipewa karatasi
Ondoa wako wasiwasi
Kokotoa kwa nafasi
Mwaswali uloulizwa

4:Sijitie mwendokasi
Machoyo' kuyapepesi
Tizamalo' karatasi
La mwenzako sitamani

5:Chuo chenu cha Huria
Hapa kwetu Tanzania
Mema kinawatakia
Mfaulu mtihani

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news