Naibu Waziri Mavunde:Tumuunge mkono Rais Samia

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri, Wizara ya Kilimo, Mhe.Anthony Mavunde amewataka wadau wote wa Kilimo kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwani ni Kiongozi anayeiangalia Sekta ya Kilimo kama njia sahihi ya kutatua changamoto za kiuchumi hasa ukosefu wa ajira kwa Watanzania.Akiongea Mei 20, 2022 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Programu ya Afrika Connection, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde amesema ili kufikia malengo ya kukuza sekta ya Kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030 serikali itashirikiana na kila mdau mwenye nia njema ya kuwanufaisha wakulima na Taifa kwa ujumla.

Mavunde ameongeza kuwa, Serikali haitashirikiana na taasisi ambayo itaonesha dalili za kudhulumu au kuwanyonya wakulima.
"Kabla ya kuja kushirikiana nanyi kwenye uzinduzi wa programu hii nilitumia muda wangu kujiridhisha kama hili suala lina maslahi kwa wakulima,"amesema Mhe. Mavunde.

Mavunde amezishauri kampuni zinazoshirikiana kwenye programu hiyo ambayo inalenga kuwawezesha wakulima wa mpunga kuanzia uzalishaji hadi kutafuta masoko, kuongeza wigo na kuwafikia wakulima wa mazao mengine ili kukuza sekta ya Kilimo na kuinua uchumi wa wakulima.
Amesema, Serikali imejidhatiti kuwekeza kwenye utafiti na uzalishaji wa mbegu ili nchi ijitosheleze kwa mbegu na ziada iuzwe nje ya nchi.

Mavunde ambainisha kuwa hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kuongeza bajeti ya umwagiliaji kutoka shilingi Bilioni 51 Mwaka 2021/2022 hadi Bilioni 361 Mwaka 2022/2023 ni kuelekea kwenye kuipa nchi uwezo wa kuendesha shughuli za kilimo bila kutegemea mvua.

Programu ya Africa Connect inalenga kuwasaidia wakulima wa mpunga kuweza kupata mikopo pamoja na huduma za miongozo ya uzalishi wa mpunga na hatimaye kuwaunganisha na masoko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news