Naibu Waziri Mavunde:Ushirika usiwe chanzo cha migogoro

NA DIRAMAKINI 

NAIBU Waziri, Wizara ya Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde ameutaka uongozi wa Ushirika kuwa wabunifu kwa kuzalisha utajiri na kuepuka kuwa chachu ya kuzalisha migogoro ndani ya Ushirika.I
Amezungumza hayo leo Mei 12, 2022 wakati akifungua Kongamano la Pili la Tafiti za Ushirika lililofanyika jijini Dodoma.
“Tukiboresha mifumo mizuri katika uwekezaji, Ushirika mna uwezo mkubwa wa kutatua changamoto zinazoikabiri nchi yetu,”amesema.

Mhe. Mavunde ametoa wito kuchukuliwa hatua wote ambao watauchafua Ushirika na kuleta sura mbaya kwa Serikali na Taifa kwa ujumla.“Watakaouchafua Ushirika wachukuliwe hatua, Ushirika sio mbaya, kila mmoja awajibike,”ameongeza.
Aidha, Naibu Waziri Mavunde, ameupongeza uongozi huo kwa mchakato wa kuanzisha Benki ya Ushirika ambapo italeta mapinduzi chanya kuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news