NECTA:Tukibaini haya tutakifuta kituo chochote cha mitihani

NA DIRAMAKINI

WATAHINIWA 95,955 kutoka shule za sekondari 841 na vituo vya kujitegemea 250 wanatarajia kuanza mitihani yao ya kumaliza Kidato ya Sita kesho Mei 9, 2022 na kumaliza Mei 27,2022.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dkt.Charles Msonde wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akifafanua kuwa,watahiniwa 9,670 kutoka vyuo 70 wamesajiliwa kufanya mitihani ya mwisho ya kozi ya ualimu katika ngazi ya Stashahada na cheti.

Amesema, baraza halitasita kukifuta kituo chochote cha mitihani endapo litajiridhisha kuwa uwepo wake unahatarisha usalama wa mitihani ya Taifa.

"Baraza linatumia nafasi hii kuwataka wamiliki wa shule wote kutambua kuwa shule ni vituo maalumu vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyaji mitihani hii," amesema Dkt.Msonde.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news