Ni wakati wa wastaafu na wanachama mifumo ya hifadhi za jamii kutabasamu, kanuni mpya ya mafao ya pensheni yaainisha

NA GODFREY NNKO

SERIKALI imesema kuwa, kanuni mpya ya mafao ya pensheni kwa wastaafu inatarajia kuongeza kiwango cha mkupuo wa mafao kutoka asilimia 25 iliyolalamikiwa mwaka 2018 hadi asilimia 33.
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nyanda Shuli akitoa inayohusu Kanuni Mpya za Kikokotoo cha mafao ya Pensheni katika Kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari Mei 27,2022 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Deodatus Balile (kushoto) akizzungumza alipokuwa akiongoza zoezi la Wahariri kuuliza maswali kwenye kikao kazi hicho.

Aidha, mshahara wa kukokokotoa mafao ya pensheni ni wastani wa mishahara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka 10 kabla ya kustaafu.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bw.Nyanda Shuli wakati akiwapitisha na kuwaelimishwa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini katika kanuni mpya ya mafao ya pensheni
inayotarajiwa kuanza Julai Mosi,2022.
Ni kupitia kikao kazi kati ya Wahariri na wataalaam mbalimbali kilichoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambacho kimefanyika leo Mei 27,2022 jijini Dodoma.

Bw.Shuli pia amesema,wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii watanufaika na ongezeko hilo kwani malipo ya mkupuo yatapanda kwa asilimia 81 ya wanachama na malipo ya pensheni yataongezeka kwa asilimia 19 ya wanachama.

Meneja Matekelezo wa PSSSF, Victor Kikoti (katikati) akizungumza alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wa kikao kazi hicho jijini Dodoma.Kulia ni mwanasheria wa NSSF Frank Mgeta, na wa pili kushoto ni Lulu Mengele ambaye ni Meneja Mahusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF.
 
"Kanuni inaongeza pensheni ya mwezi kutoka asilimia 50 ya sasa hadi asilimia 67 kwa wanachama wa PSPF na LAPF.

Mkurugenzi wa Adhari wa PSSSF, Ansiger Mushi (kulia aliyesimama) akizungumza kwenye kikao kilichoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa wahariri wa vyombo vya habari jijini Dodoma.

"Kanuni itaweka uwiano na usawa wa mafao baina ya wastaafu wote na itafanya mifuko kuwa imara na endelevu,"amesema Bw.Shuli.
Meneja Mahusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele akizungumza alipokuwa akifafanua jambo wakati akijibu maswali ya wahariri katika kikao kazi hicho cha Mei 27,2022 jijini Dodoma.
 
Kamishna huyo amefafanua kuwa, kazi iliyofanyika kwa ushirikiano wa Wadau wa Utatu kwa maana ya Serikali,Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) imewezesha kupata kanuni bora na endelevu.

Kwa nini hifadhi ya jamii
Bw.Shuli amefafanua kuwa, Hifadhi ya Jamii inaimarisha ustawi wa jamii kwa kuweka mifumo inayowakinga wananchi dhidi ya majanga ya kijamii kama vile uzee, ulemavu, kifo, ugonjwa na kukosa ajira.

"Ipo mifumo ya uchangiaji au isiyo ya uchangiaji (misaada).Mifumo ya uchangiaji ina wanachama wanaochangia na hivyo kustahili huduma kulingana na sheria na kanuni zinazotumika.
Meneja Matekelezo wa PSSSF Victor Kikoti (katikati) Akizungumza alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wa kikao kazi hicho Jijini Dodoma. (kulia) ni mwanasheria wa NSSF Frank Mgeta, na (wa pili kushoto) ni Lulu Mengele Meneja Mahusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF.
 
"Mifumo ya uchangiaji inaipunguzia Serikali mzigo kupitia bajeti ya Serikali,"anafafanua Bw.Shuli.

Anaongeza kuwa,mifumo isiyo ya uchangiaji (misaada) ni kama vile TASAF na huduma za afya kwa wazee na makundi mengine.

Pia amesema mifumo hiyo inatambuliwa kimataifa ikiwemo kupitia Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu (1948).
Mkataba wa Usalama wa Jamii wa ILO (Viwango vya Chini), 1952 (Na.102) Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (1966) Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu.

Pia inatambuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) na sheria Ibara ya 11(1).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news