Sehemu ya wajumbe wa kikao kazi cha kukamilisha Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa Wilaya ya Kyela wakijadiliana wakati wa kazi za makundi.
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. SACP Ismail Mlawa akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Wataalam wa Wilaya hiyo, kilicholenga kukamilisha Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa katika Wilaya hiyo Jijini Mbeya. Kikao kiliratibiwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu na kufanyika tarehe 24 Mei, 2022.
Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Ally Mwatima akiwapitisha wajumbe wa kikao kazi hicho (hawapo pichani) wakati wa kuujadili Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.
Mratibu wa Maafa Mkoa wa Mbeya Bw. Juma Maduhu akifafanua jambo wakati wa kikao kazi hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. SACP Ismail Mlawa (wa pili kulia waliokaa) pamoja na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi wa kikao kazi cha kukamilisha Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa Wilaya hiyo. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).