NA DIRAMAKINI
CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu katika nafasi ya Rais, Makamu wa Rais na Mweka Hazina.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Mei 27, mwaka huu jijini Arusha, ambapo tayari kampeni za wagombea urais zimeanza tangu Aprili 15, mwaka huu na zinatarajiwa kuhitimishwa Mei 26, mwaka huu siku ambayo pia utafanyika uchaguzi katika nafasi nyingine ikiwemo ya viongozi wa kanda.
"Baraza zima la uongozi la TLS litazingatia suala la usawa wa kijinsia katika maamuzi na shughuli zote.
"Kama tulivyoonyesha katika uongozi wa mwaka mmoja uliopita, tutaendelea kutekeleza mipango inayotambua nafasi ya mwanamke katika jamii ili kuleta usawa wa kijinsia utakao toa nafasi sawa kwa makundi yote katika jamii,"anasema mgombea Urais wa Tanganyika Law Society, Prof.Edward Hoseah.
Wanasemaje kuhusu Profesa Edward Hoseah (VIDEO)
"Mimi ni mwanasheria, wakili na pia wakili kiongozi wa Kampuni ya Wanasheria. Ni mwanachama wa TLS, tunajiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu, kwa nafasi yangu ndani ya chama pamoja na mbele ya wanajamii kwa ujumla, ningeomba kwa heshima kuwaomba wanachama wenzangu wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS) pamoja na wapiga kura wote ambao watashiriki katika zoezi la upigaji kura katika nafasi mbalimbali,lakini hasa katika kiti cha mgombea Urais wa Kiti wa Chama cha Wanasheria. Tumchague Profesa Edward Hoseah kutokana na umuhimu wa Profesa katika uchaguzi huu, lakini pia katika chama chetu cha mawakili"
"Mawakili na wote wanaohusika katika kwachagua viongozi wa mawakili,waweze kumchagua tena Profesa Edward Hoseah apate nafasi nyingine ya kuongoza jopo hili, kwani tumeshuhudia uongozi uliotukuka, uliokuwa na utulivu wa hali ya juu, mawakili walikuwa na utulivu, wamefanya kazi zao kwa weledi wa hali ya juu,utulivu, hivyo siyo mbaya, ningependa kusisitiza wote wampe nafasi tena aweze kutuvusha katika kipindi kingine".
"Kwa kipindi chote ambacho Profesa Hoseah alikuwa Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania, nimekuwa nikimfuatilia kwa kina ni namna gani anaongoza chama hiki, tumeona alikuwa ni kiongozi bora,alikuwa akiongoza watu katika kufuata misingi, haki na sheria,ni kiongozi mwenye hekima,shupavu, busara, mtulivu".
Kwa nini umchague Prof.Edward Hoseah?
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ambaye anatetea kiti chake, Profesa Edward Hoseah ni kati ya viongozi ambao wamefanikiwa kushirikiana na wenzake kuiendesha taasisi hiyo kwa mafanikio makubwa ndani ya mwaka mmoja.
Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kuishawishi Mahakama Kuu ya Tanzania kurejeshewa tozo ya shilingi milioni 450 ambazo tangu Uhuru walikuwa wakilipa mahakama kama ada.
Pia kupitia uongozi wake amefanikiwa kupunguza ada ya uwakili kutoka shilingi 60,000 hadi shilingi 20,000, kupunguza gharama ya afya kutoka shilingi milioni 1,050,000 hadi shilingi 500,000, kuimarisha uhusiano baina ya taasisi hiyo na Serikali ambao umeonesha nuru kubwa na mengineyo mengi.
Licha ya uzoefu mkubwa katika uongozi na ubobezi wa kutosha katika sheria, Profesa Hoseah ni miongoni mwa Watanzania wanaoipenda TLS, anaamini kupitia uongozi wake kwa kushirikiana na wenzake wanaweza kuistawisha zaidi taasisi hiyo muhimu.
Mfahamu kwa kina Profesa Edward Hoseah hapa;