NA DIRAMAKINI
RAIS wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ambaye anatetea kiti chake, Profesa Edward Hoseah ni kati ya viongozi ambao wamefanikiwa kushirikiana na wenzake kuiendesha taasisi hiyo kwa mafanikio makubwa ndani ya mwaka mmoja. Kwa asilimia kubwa amefanikiwa kutekeleza ahadi za mwaka 2021-2022 kama ifuatavyo;
HUDUMA NA USTAWI WA WANACHAMA
1. Tumeweza kuboresha Huduma za Msaada wa Kisheria kwa kufanya yafuatayo
2. Tumepanua wigo wa utoaji wa msaada wa kisheria kutoka kuwa zoezi la wiki moja mpaka kuwa zoezi la kudumu.
3. Tumefanikiwa kushawishi serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kutoa ruzuku ya TZS 1.2 bilioni kwa TLS kwa ajili ya kufanikisha zoezi la kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi.
4. Tumefanikiwa kushiriki katika mashauri mbalimbali chini ya mpango wetu wa huduma za msaada wa kisheria na chini ya mpango wa mashauri yenye maslahi ya umma.
USHIRIKANO NA WADAU MBALIMBALI