NA ANGELA MSIMBIRA, OR-TAMISEMI
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Prof. Riziki Shemdoe amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri 59 kuhakikisha wanarejesha fedha za bakaa na kujibu hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Prof. Shemdoe amefafanua kuwa, katika ukaguzi uliofanywa na CAG katika mwaka wa fedha 2020/21 hoja kubwa ni halmashauri hizo kutumia fedha kwenye kazi sahihi lakini na kuahindwa kuziripotia ipasavyo.

Aidha, halmashauri zilifanya malipo ya Dummy Exchequer kwenda kwenye vituo vya afya na zahanati ikiwa mgawanyo ulishapelekwa na hazina pamoja na malipo kuvuka mwaka mwingine wa fedha,

Amezitaka halmashauri hizo kuhakikisha zinarejesha fedha hizo kwa wakati na kufanya usuluhishi wa kifedha kwa kutoa nyaraka zinazotakiwa ili hoja hizo zimalizike kwa wakati na kama fedha zilitumika na kutakiwa kurejeshwa za mapato ya ndani ni kiasi gani kilitakiwa kurejeshwa.