NA ANGELA MSIBIRA,OR-TAMISEMI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa kusimamia tenda za ununuzi wa vifaa tiba na kazi zingine kupitia fedha za UVIKO-19.

Mhe.Rais Samia anafafanua kuwa, mwisho wa matumizi ya fedha za UVIKO-19 ni mwezi Juni, 2022 hivyo fedha zote zinahitajika kutumiwa kwa wakati ili kukidhi vigezo vya kuoa fedha zaidi, amemuagiza Waziri Bashungwa kuhakikisha zabuni hizo zinafanyiwa kazi kwa wakati ili kazi hizo zikamilike kwa wakati.

Kuhusu matumizi ya fedha kwenye Halmashauri Rais Samia ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatumia fedha zinazotolewa na Serikali kwa kazi zilizokusudiwa za kutatua kero za wananchi

Aidha, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa matundu ya vyoo, meza, ujenzi wa maabara, ununuzi wa viti na ujenzi wa nyumba za waalimu.