NA DIRAMAKINI
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
ameridhia mapendekezo ya kuongeza mishahara ikiwemo kima cha chini kwa
watumishi wa umma kwa asilimia 23.3, ambapo shilingi trilioni 1.59
itatumika kwa ongezeko hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 14, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.
Taarifa
hiyo inasema, mapendekezo hayo ni mwendelezo wa kikao cha Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa alichokifanya hivi karibuni mkoani Dodoma na kupokea
taarifa kutoka kwa wataalamu kuhusu ongezeko la mishahara.
Pia
taarifa hiyo imesema Serikali imepanga kutumia kiasi cha shilingi
trilioni 9.7 katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya kugharamia
malipo ya mishara ya watumishi wote katika Serikali Kuu, Serikali za
Mitaa, Taasisi na Wakala za Serikali.
“Bajeti
ya mishahara ya mwaka 2022/23 inaongezeko la shilingi trilioni 1.59
sawa na asilimia 19.51 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha wa
2021/22,” imefafanua taarifa hiyo.
Sekta binafsi ni watumishi lakini kwa serikali ya jamuhuri ya mungano wa Tanzania awatambuliki .ata mama yetu ameshindwa kuwaongelea ongezeko la mishaara mipya.
ReplyDelete