NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan leo Mei 31, 2022 amezindua kitabu cha mwanamuziki nguli wa Hip Hop, Mr 2 Proud au maarufu kama Sugu kiitwacho muziki na maisha kwenye tamasha la kutimiza miaka 30 katika tasnia hiyo.

Tamasha hili limepambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sugu mwenyewe ambaye ametumbuiza na kukonga nyoyo za mamia ya watu waliohudhuria.
Mhe. Rais amemtunukia tuzo, Sugu huku akimpongeza kuwa miongoni wasanii wenye nyimbo zenye maadili.