NA TITO MSELLEM-WM
SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuonesha dhamira yake ya kutengeza mabilionea na mamilionea wapya kwa kuwapatia fursa ya kuchimba madini kwa kuwaongoza vyema kuelekea kwenye mafanikio.
Waziri Biteko amesema Soko Kuu la Mkoa wa Mwanza limeuza na kununua jumla ya tani tisa za madini ya dhahabu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Sambamba na hayo, Dkt. Biteko amesema Kampuni ya Busolwa imenya uwekezaji unaopaswa kuigwa na wawekezaji wengine ambapo kampuni hiyo imeweka mfumo wa uwekezaji kwa kuwahusisha wananchi wa kawaida kupitia umoja wao wa Isihika ambapo wana asilimia 20 na mwekezaji kampuni ya Busolwa asilimia 80.

Kuhusu uanzishwaji wa masoko ya madini, Dkt. Biteko amesema yamesaidia kurahisisha biashara na kupunguza changamoto ya utoroshaji madini ambapo amebainisha kuwa kwa Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi kufikia Mwezi Machi Mwaka huu kiasi cha tani tisa ya dhahabu imeuzwa katika Soko Kuu la Madini mkoani wa Mwanza na hivyo kuwapongeza wachimbaji kwa ushirikiano wao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy amewahakikishia wawekezaji katika mgodi wa Busolwa kutengeneza mazingira rafiki ya uwekezaji katika wilaya hiyo.