NA OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa ametoa siku 30 kwa Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam kufanya upembuzi yakinifu wa barabara Suca-Golani katika Wilaya ya Ubungo yenye urefu wa kilomita 7.5 ili itengewe bajeti na kujengwa kwa kiwango cha lami.
Bashungwa ametoa maagizo hayo kwa Meneja huyo, Mhandisi Geofrey Mkinga wakati wa ziara katika wilaya ya Ubungo ya kukagua barabara ya Suca - Golani inayohudumia kata mbili ya Saranga (Jimbo la Kibamba) na Kata ya Kimara (Jimbo la Ubungo).
Amesema, baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasaan kusikia kilio cha muda mrefu cha mawasiliano, barabara hiyo amemuagiza kufika katika eneo hilo na kuhakikisha anatatua kero hiyo ya wananchi.
Waziri Bashungwa amemuagia Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Ubungo kupitia asilimi 60 ya mapato ya ndani inayotengwa kutekeleza miradi ya maendeleo na asilimia 10 kati ya hiyo inayotengwa kwa ajili ya barabara kulingana na Mwongozo wa Ofisi ya Rais TAMISEMI atenge fedha ambazo atashirikiana na TARURA ili kujenga barabara hiyo.
Aidha, Bashungwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita itahakisha inatatua kero za wananchi wote bila kujali mijini au vijijini ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapindunzi.
Pia ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikao kwa timu itayokuwa inafanya upembuzi yakinifu ili wakamilishe kazi hiyo wa wakati ya kupata BOQ ili Serikali iweze kuleta fedha za kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.