NA DIRAMAKINI
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imetoa tahadhari kwa watendaji wa serikali wanaoshirikiana na matapeli wa ardhi na kusisitiza kuwa dawa yao wanayo.

Myava amesema kuwa, baadhi ya matapeli wa ardhi wamekuwa wakitumia vitendo vya rushwa na kusababisha migogoro isiyokwisha ambayo iko mahakamani.
Amesema kuwa, baadhi ya watendaji wa serikali wanaojihusisha na vitendo vya rushwa kwa kushirikiana na matapeli wajue wanawafuatilia ili kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Kwa upande wa rushwa kwenye chaguzi za ndani za vyama amesema, watazifuatilia ili kukabiliana na viongozi wanaotoa rushwa kupata uongozi kwani ni kinyume cha sheria.
Ameongeza kuwa, kwenye chaguzi hizo na hawatakaa nyuma bali watajikita katika kutoa elimu juu ya madhara ya rushwa ili wananchi waweze kuchagua viongozi safi wasiyotokana na rushwa.