TAMISEMI Queens mmetuheshimisha sana Afrika Mashariki, hongereni-Prof.Shemdoe

NA OR-TAMISEMI

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe ameipongeza timu ya mpira wa netiboli TAMISEMI Queens kwa kuibuka washindi wanne katika mashindano ya mchezo wa netiboli Afrika Mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya Kamokya nchini Uganda hivi karibuni.
Prof. Shemdoe amesema kuwa ushindi huu haujapeperusha bendera kwa Ofisi ya Rais -TAMISEMI pekee bali kwa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania hususani katika nyanja ya michezo hivyo ameipongeza timu hiyo kwa kuwa wazalendo na kuiwakilisha vyema Tanzania na kuitaka timu hiyo kuendeleza jitihada ili kushiriki katika mashindano yajayo.

Pongezi hizo zimetolewa Mei 17,2022 katika viunga vya Ofisi ya Rais-TAMISEMI baada ya timu ya TAMISEMI Queens kuwasili ikitokea nchini Uganda kushiriki mashindano ya mchezo wa netiboli Afrika Mashariki ambapo timu ya TAMISEMI Queens ilifanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali na kuibuka washindi wanne.
Pamoja na pongezi hizo Shemdoe amewataka washiriki wa timu ya TAMISEMI Queens kutumia fursa ya ushiriki wa mashindano nje ya nchi katika kujikuza kimichezo lakini pia waitumie na fursa hiyo kama njia mojawapo ya kujiinua kiuchumi katika kuleta maendeleo nchini.

“Kwanza niwapongeze sana , mmekuwa wazalendo na mmewatuwakilisha vyema, lakini tumieni fursa hizi katika kukua sio kimichezo pekee lakini pia tumieni fursa hizi katika kukua kiuchumi,” Prof.Shemdoe.
Kwa niaba ya Timu hiyo Kempteni wa Timu ya netiboli ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI Bi. Dafroza Luhwagu ameishukuru Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na timu hiyo kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mashindano na amehaidi kuongeza jitihada katika mashindano yajayo.
Akitoa taarifa ya ushiriki wa TAMISEMI Queens katika Mashindano hayo , Katibu wa TAMISEMI Sports Club Bw. Alex Moris amesema kuwa timu hiyo imeshiriki mashindano ya mchezo wa netiboli Afrika Mashariki katika viwanja vya Kamokya nchini Uganda kuanzia tarehe 8 hadi 14 Mei ambapo timu hiyo ilifanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news