NA OR-TAMISEMI
WAKALA wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) mkoani Njombe umekamilisha ujenzi wa daraja linalounganisha kata za Ramadhani na Njombe Mjini ambalo kilikuwa hatari kwa watumiaji kutokana na kutandikwa matapa.
Awali watumiaji wa daraja hilo wanasema madereva wa vyombo vya moto na wanafunzi walikuwa wakitumbukia mtoni wakati wa mvua kubwa ambazo zilikuwa zikifunga njia.
Kutokana na hali hiyo mwanzoni mwa mwaka huu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa alifikuwa katika daraja hilo na kumtumbua aliyekuwa Meneja wa TARURA mkoani humo kisha kuhamishiwa Mkoa wa Ruvuma kwa kuchelewa kutekeleza mradi huo uliokua umeshapatiwa fedha kipindi alipokuwa mkoani Njombe kabla ya kuhama.
Hivi sasa wananchi wanafurahia ujenzi huo ambapo wanasema imerahisisha usafiri kwa wao kuweza kusafirisha biashara zao na kuongeza usalama kwa wote wanaotumia barabara hiyo.