NA MWANDISHI WETU
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewahamasisha wananchi kutembelea banda lake katika Maonesho ya Tisa ya Biashara na Utalii yanayoendelea katika Uwanja wa Mwahako jijini Tanga ili kupata huduma mbalimbali. Maonesho hayo ambayo yalianza Mei 28, 2022 yanatarajiwa kufikia tamati Juni 6, 2022.





Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi mapema leo na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji ( Mb).