NA ASILA TWAHA,OR-TAMISEMI
WASHIRIKI wa Mafunzo Endelevu Kazini (MEWAKA) wameiomba Serikali kuendelea kuvisimamia na kuviwezesha vituo vya MEWAKA katika shule ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi na kwa kupitia vituo hivyo walimu waeleze changamoto zao.

Mwakasembe amesema, pamoja na kuchelewa kwa mafunzo hayo wanaishukuru Serikali kuona ni muhimu walimu kupatiwa mafunzo kwa lengo la kuwajengea uwezo na jinsi ya kuviendeleza vituo vya MEWAKA shuleni.
Aidha, amesema walimu itawasaidia kujifunza, kutatua changamoto na kupata maarifa mapya wanapokutana watabadilisha uzoefu na kushauriana sababu kazi ya ualimu kila siku unatakiwa uwe ana mbinu mpya za ujifunzaji na ufundishaji.

“Tunaiomba Serikali kuendelea kuviwezesha na kuvipa nguvu vituo vya MEWAKA katika suala la usimamizi wa kufuata sheria, taratibu na miongozo ili visije vikasimamishwa,"amesema.
"Ili Serikali ipate maendeleo katika uboreshaji wa elimu nchini ni lazima vituo hivyo kuvisimamia sababu vitawasaidia kujua changamoto za elimu nchini” amesema Mwakasembe.
Aidha, ameiomba Serikali kuendelea kuisimamia sekta ya elimu kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu ikiwa wao walimu wa shule za awali na msingi ndio msingi elimu wapo tayari kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi waliopewa jukumu la kuwasimamia.
Naye Mwalimu Levina Mwanchang’a mshiriki wa mafunzo kutoka Shule ya Msingi Senga amesema, mwanzo walikuwa wanafundisha kwa uzoefu mwalimu hana mbinu mpya za kufundishia bila kujua kuna mabadilko katika ujifunzaji na ufundishaji kwa kupata mafunzo hayo yanaenda kuwasaidia kuongeza ujuzi na maarifa.

Kwa upande wa Mratibu wa Halmashuri ya Wilaya ya Kaliua, Mwalimu Matuna Massati amesema, jumla ya washirki 226 wameshiriki na tathmini wanayoendelea kuifanya baada ya mafunzo imeonyesha walimu wapo makini.
Kwa sababu lengo la mafunzo hayo yanayoendelea ni kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao, Serikali inaamini kumalizika kwa mafunzo hayo walimu wataenda kuwa viongozi bora katika utekelezaji wa kazi zao.