*TMA INATOA ANGALIZO KUHUSU HALI YA UPEPO MKALI UNAOFIKIA KILOMITA 40 KWA SAA KWA BAADHI YA MAENEO YA UKANDA WA PWANI YA BAHARI YA HINDI
NA GODFREY NNKO
UTABIRI wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku leo Mei 2,2022 unaletwa na mchambuzi Daniel Masunga kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA,Mikoa ya Kigoma, Katavi, Kagera, Geita, Mwanza na Mara inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua
Aidha, visiwa vya Unguja na Pemba vinatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) kwa mujibu wa TMA, inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Huku mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Morogoro, Dodoma, Singida, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya ikitarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Wakati huo huo, TMA inatoa angalizo la upepo mkali unaofikia Kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 katika baadhi ya maeneo Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi ikijumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Pwani (visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Unguja na Pemba.
TANZANIA WEATHER FORECAST 02.03.2022:STRONG WIND REACHING 40KM/HR IS EXPECTED FOR SOME AREAS ALONG THE COAST OF THE INDIAN OCEANWeather forecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight 02.05.2022, presented by weather analyst Daniel Masunga from Tanzania Meteorological Authority (TMA).