NA GODFREY NNKO
LEO Franka ya Ubeligiji (BEF) inanunuliwa kwa shilingi 50.06 na kuuzwa kwa shilingi 50.51 huku Pula ya Botswana (BWP) ikiuzwa kwa shilingi 188.5 na kununuliwa kwa shilingi 191.7.
Yen ya Japan (JPY) inanunuliwa kwa shilingi 17.6 na kuuzwa kwa shilingi 17.8 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 144.4 na kuuzwa kwa shilingi 145.8.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Mei 2, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65 huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.
Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2287.4 na kuuzwa kwa shilingi 2310.3 huku Paundi ya Uingereza (GBP) ikinunuliwa kwa shilingi 2870.7 na kuuzwa kwa shilingi 2900.1.
Aidha,Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2411.65 na kuuzwa kwa shilingi 2436.7 huku Yuan ya China (CNY) ikinunuliwa kwa shilingi 347.31 na kuuzwa kwa shilingi 350.6.
Kwa mujibu wa BoT, shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.8 na kuuzwa kwa shilingi 19.9 huku Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.22 na kuuzwa kwa shilingi 2.29.
Dirham (AED) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inanunuliwa kwa shilingi 622.8 na kuuzwa kwa shilingi 628.9 huku sarafu ya Austria ya Schilling (ATS) inanunuliwa kwa shilingi 146.8 na kuuzwa kwa shilingi 148.1.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania