NA GODFREY NNKO
LEO Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 337.14 na kuuzwa kwa shilingi 340.36 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 17.7 na kuuzwa kwa shilingi 17.9.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Mei 16, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kwa upande wa Paundi ya Uingereza (GBP) inanunuliwa kwa shilingi 2792.25 na kuuzwa kwa shilingi 2820.40 huku Dola ya Marekani (USD) ikinunuliwa kwa shilingi 2288.17 na kuuzwa kwa shilingi 2311.05.
Aidha, Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2377.18 na kuuzwa kwa shilingi 2401.8.
Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini (ZAR) inanunuliwa kwa shilingi 141.8 na kuuzwa kwa shilingi 143.2 huku shilingi ya Kenya (KES) ikinunuliwa kwa shilingi 19.7 na kuuzwa kwa shilingi 19.9.
Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.21 na kuuzwa kwa shilingi 2.27 huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 21.
Kwa upande wa shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.61 na kuuzwa kwa shilingi 0.64 huku Franka ya Ubelgiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.08 na kuuzwa kwa shilingi 50.53.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania