NA GODFREY NNKO
LEO Kwacha ya Malawi (MWK) inanunuliwa kwa shilingi 2.6 na kuuzwa kwa shilingi 2.8 huku Metical ya Msumbiji (MZM) ikinunuliwa kwa shilingi 35.3 na kuuzwa kwa shilingi 35.6.
Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 343.8 na kuuzwa kwa shilingi 347.16 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 17.9 na kuuzwa kwa shilingi 18.1.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Mei 24, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Won ya Korea Kusini (KRW) inanunuliwa kwa shilingi 1.81 na kuuzwa kwa shilingi 1.83 huku Dinar ya Kuwait (KWD) ikinunuliwa kwa shilingi 7482.3 na kuuzwa kwa shilingi 7546.8.
Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.60 na kuuzwa kwa shilingi 0.63 huku Franka ya Ubelgiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.09 na kuuzwa kwa shilingi 50.54.
Kwa upande wa Paundi ya Uingereza (GBP) inanunuliwa kwa shilingi 2876.9 na kuuzwa kwa shilingi 2906.7 huku Dola ya Marekani (USD) ikinunuliwa kwa shilingi 2288.8 na kuuzwa kwa shilingi 2311.7.
Aidha, Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2427.5 na kuuzwa kwa shilingi 2452.7 huku Rupia ya Pakistan (PKR) ikinunuliwa kwa shilingi 10.8 na kuuzwa kwa shilingi 11.5.
Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini (ZAR) inanunuliwa kwa shilingi 144.9 na kuuzwa kwa shilingi 146.3 huku shilingi ya Kenya (KES) ikinunuliwa kwa shilingi 19.7 na kuuzwa kwa shilingi 19.8.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania
Uchumi na Biashara