NA GODFREY NNKO
LEO Franka ya Burundi (BIF) inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku Franka ya Rwanda (RWF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.22 na kuuzwa kwa shilingi 2.29.
Dola ya Zimbabwe (ZWD) inanunuliwa kwa shilingi 0.43 na kuuzwa kwa shilingi 0.44 huku Shilingi ya Uganda (UGX) ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Mei 9,2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Aidha, shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.7 na kuuzwa kwa shilingi 19.9 huku Euro ya Ulaya (EUR) ikinunuliwa kwa shilingi 2422.4 na kuuzwa kwa shilingi 2447.6.
Aidha, Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2287.7 na kuuzwa kwa shilingi 2310.6 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 143.1 na kuuzwa kwa shilingi 144.3.
Kwa upande wa Kwacha ya Zambia (ZMK) inanunuliwa kwa shilingi 133.4 na kuuzwa kwa shilingi 135.7 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.07 na kuuzwa kwa shilingi 50.52
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania