NA DIRAMAKINI
“Naomba nichukue fursa hii kuwataka wadau wote wa madini hususani viongozi katika migodi yote nchini na maeneo yenye shughuli za madini kuhakikisha wanashiriki katika uhamasishaji na uelimshaji juu ya umuhimu wa sensa katika kupanga mipango ya kitaifa.
"Sensa inayotegemea kufanyika 2022 chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni Sensa ya Sita tokea nchi imepata uhuru wake mwaka 1961 iliyobebwa na kaulimbiu ya “Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa,"alisema Waziri wa Madini, Dkt.Doto Biteko katika hafla ya Uzinduzi wa Mpango wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 iliyofanyika Septemba 14, 2021 katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.