NA DIRAMAKANI
WAKATI Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) akimaliza kipindi cha kwanza huku akiomba tena nafasi hiyo kupitia Uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika wiki hii, Prof. Edward Hoseah baadhi ya Wanasheria na Maafisa wa Dawati la Jinsia wameeleza kuridhishwa na uongozi wake na kusema umeleta matunda chanya ya utatuzi wa migogoro na kuimarisha mwenendo thabiti wa ushirikiano na vyombo mbalimbali katika usimamizi wa sheria nchini.
Hayo wameyabainishwa kwa nyakati tofauti ambapo wameeleza matumaini yao kuwa, kutokana na uwajibikaji wake madhubuti katika kipindi kilichopita bado ana nafasi kubwa ya kuendelea kukiongoza chama hicho kwa ufansi.
Hivyo, wamewaomba Wanasheria na Mawakili wampe ridhaa kwa kumchagua tena katika Uchaguzi utakaofanyika Mei 27, 2022 kusudi aendeleze harakati chanya za kuzidi kukijenga chama, kukiimarisha na kufikia malengo yaliyokusudiwa.
"Mchango wa Profesa Hoseah umeweza keleta matunda chanya katika utatuzi wa migogoro hasa namna gani ambavyo katika mhimili wa sheria katika nchi yetu unavyoenenda na ulivyoweza kulinda maslahi ya wananchi kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali katika usimamizi wa sheria nchini.
"Hivyo, niwaombe Wanasheria na Mawakili ambao wanakwenda kufanya uchaguzi siku ya Ijumaa tuweze kumpa ridhaa Profesa Hoseah aweze kuendeleza Constructive Engagement katika nyanja ya kisheria ambayo inahitaji mambo ya kushirikiana na taasisi mbalimbali katika kuhakikisha kwamba yale malengo yanaweza kufikiwa,"amesema Pertnus Pascal Shauri.
Kwa upande wake Koplo Mwajabu ambaye ni Askari Polisi Kitengo cha Dawati la Jinisia na Watoto Mkoa wa Kilimanjaro amesema kuwa, "kwa uongozi ambao upo sasa hivi Wanasheria wanajitambua na hawadanganyi wateja wao, wanashirikiana na Jeshi la Polisi kutokana na ushirikiano uliopo baina ya Polisi na Wanasheria katika kuandaa kesi kwa sababu tunashirikiana yaani kesi za dawati zinapokuwa zimetokea tunaziandaa lazima ianzie polisi na polisi tuwapelekee wanasheria,"amesma.
"Kwenye Uongozi wa Profesa Hoseah mambo ni mazuri, hakuna makando kando kama ni kesi, kesi zimenyooka, tukiandaa jalada letu likienda kule kwa umoja linafanyiwa kazi na mwisho wa siku linatendewa kazi na mwisho tunapata mwafaka, kwa hiyo tunashukuru sana maana Consructive Engagement naona mambo si mabaya yako vizuri, kwa hiyo tunampongeza sana, Mungu azidi kumpigania,"amesema Koplo Mwajabu.
Mfahamu kwa kina Profesa Edward Hoseah hapa;