NA DIRAMAKINI
WANANCHI wa maeneo mbalimbali ya jijini Mbeyal leo Mei 31, 2022 wameshiriki Kongamano la Kuliombea Taifa pamoja na kumuombea na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi bora tangu aingie madarakani.
Katika Kongamano lililoongozwa na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini pia ilishuhudia Rais Samia akizungumza na watanzania kupitia Kongamano hilo kwa njia ya simu ambapo amewaahidi kuendelea kuwatumikia kwa maslahi mapana ya Taifa.